Na. A/insp. Nurdin Nanyanga.
Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Sayansi ya Urekebishaji Tanzania (TCTA) kilichopo Ukonga jijini Dar es salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Willington Kahumuza, Mapema leo Oktoba 04, 2024 amekabidhiwa gari mpya aina ya Toyota Land Cruiser Hard top na Mkuu Msaidizi wa Kitengo cha Usafirishaji cha Jeshi la Magereza Mrakibu wa Magereza (SP) Adam Kipalamoto, kwaniaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza Jeremiah Yoram Katungu.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya gari hilo , Mkuu wa Chuo SACP. Kahumuza amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzani Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi la Magereza vitendea kazi.
Aidha amemshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni (MB) na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Jeremiah Yoram Katungu kwa kuwapa kipaumbele kwa Chuo TCTA katika Mgao wa gari
Aidha amewataka Watumishi wa Chuo kulitunza gari hilo ili liweze kudumu na kufanya kazi zilizokusudiwa.