Monday, October 20, 2014

TANZIA

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
(Jeshi la Magereza)

TANZIA
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi, Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Stephen J.K. Nzawila kilichotokea Jijini Dares Salaam tarehe 19 Oktoba, 2014.

Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Familia ya Marehemu linaratibu mazishi yake ambapo mwili wa marehemu utaagwa rasmi leo tarehe 20 Oktoba, 2014 saa 10:00 jioni nyumbani kwake Magereza Ukonga, Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Tutuo Wilayani Sikonge, Mkoani Tabora kwa mazishi.

          Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi;
AMINA