Monday, June 12, 2017

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWAVISHA VYEO MAAFISA WAANDAMIZI WA MAGEREZA KWA NIABA YA RAIS, AHIMIZA HAKI NA USAWA MAGEREZANI

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa salaam ya heshima kwa Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa alipowasili kwenye hafla ya  kuwavalisha Vyeo Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt. John Pombe Mgufuli katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akipokea salaam ya heshima kutoka kwa gwaride maalum katika hafla fupi ya kuwavalisha Vyeo Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akikagua gwaride katika hafla fupi ya kuwavalisha Vyeo Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt. John Pombe Mgufuli katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akimvalisha cheo Tusekile Mwaisabila kuwa Naibu Kamishina wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika  hafla hiyo .
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akimvalisha cheo, Afwililwe Mwakijungu kuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akimvalisha cheo, Joel Bukuku kuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017.
Maafisa wandamizi wa Jeshi la Magereza wakisoma Tamko la Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma baada ya kuvalishwa vyeo na Waziri Mkuu, Mhe. Kasim Majaliwa katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba fupi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni aweze kumkaribisha Waziri Mkuu Mhe. Kasim Majaliwa ili aweze kuongea machache kwenye hala hiyo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni akitoa neno kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu Mhe. Kasim Majaliwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika hafla fupi ya kuvalisha vyeo Maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017.
Maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza waliopandishwa vyeo na Mhe. Rais Magufuli akifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu.
Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kutoka maeneo ya jirani na Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam wakifuatilia tukio hilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa magereza aliowavalisha Vyeo kwa Niaba ya Rais John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni, 12, 2017. Walioketi(wa tatu toka kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa tatu toka kulia) ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni 
(Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano – Jeshi la Magereza).


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka maaafisa na makamanda wote wa Jeshi la Magereza nchini kuendelea  kusimamia haki na usawa wanapotimiza wajibu wao wa kila siku.

Ametoa wito huo leo jioni (Jumatatu, Juni 12, 2017) wakati akizungumza na maafisa na makamanda wa jeshi hilo katika hafla ya kuwavisha vyeo maafisa waandamizi wa magereza 29 iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA), Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ambaye amefanya kazi hiyo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amewavisha vyeo maafisa waandamizi wa magereza watano kuwa Manaibu Kamishna wa Magereza (DCP) na maafisa waandamizi wa magereza 24 kuwa Makamishna Waandamizi Wasaidizi wa Magereza (SACP). Maaafisa hao walipandishwa vyeo na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Mei 25, mwaka huu.

“Ninyi ni viongozi wakuu katika mikoa mnayotoka. Huko kuna makamanda walio chini yenu na jamii inayowazunguka. Endeleeni kuwahudumiana na kulitumikia Taifa hili kwa weledi mkubwa. Endeleeni kusimamia usawa na haki katika kazi zenu za kila siku,” amesema.

Waziri Mkuu amesema hana shaka na utendaji kazi wa jeshi la Magereza kwani watumishi wake ni waadilifu. “Jeshi hili linayo nidhamu ya hali ya juu, mbali ya jukumu lenu la ulinzi, mnafanya kazi nidhamu, weledi na uadilifu mkubwa,” amesema.

Amesema Serikali inatambua changamoto zinazowakabili katika utendaji wao wa kila siku na kwamba inajitahidi kuzishughulikia hasa baada ya kukamilisha zoezi la kuondoa watumishi hewa.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuhutubia maafisa hao, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Yusuph Masauni amewataka maafisa waliovishwa vyeo hivyo wazingatie maadili ya kazi zao na uzalendo kama ambavyo wameapa kwenye kiapo cha maadili.

Maafisa Waandamizi watano waliovalishwa vyeo kuwa Naibu Kamishna wa Magereza ni SACP Uwesu Ngarama; SACP Gideon Mkana (Mkuu wa Chuo cha TCTA); SACP Jeremiah Nkondo (RPO-Kagera); SACP Tusekile Mwaisabila (RPO-Lindi) na SACP Augustine Mboje (RPO-DSM).

Maafisa Waandamizi  24 waliovalishwa vyeo kuwa Makamishna Waandamizi Wasaidizi wa Magereza (SACP) ni ACP Mbaraka Semwanza; ACP George Mwambashi; ACP Charles Novati; ACP Faustine M. Kasike; ACP Joel Bukuku; ACP Deogratius Lwanga; ACP Boyd P. Mwambingu (RPO Pwani); ACP Athumani Kitiku (RPO Mwanza) na ACP Hassan Mkwiche (RPO Kilimanjaro).

Wengine ni ACP Luhende D. Makwaia; ACP Hamza R. Hamza; ACP Jeremiah Y. Katengu; ACP Mzee R. Nyamka (Kaimu RPO Morogoro); ACP Afwilile Mwakijungu (Mkuu wa gereza la Isupilo, Iringa); ACP Ali Kaherewa (Kaimu RPO Singida); ACP Ismail Mlawa (RPO Mtwara); ACP Chacha B. Jackson; ACP Rajab N. Bakari; ACP Kijida P. Mwankingi; ACP Julius C. Ntambala; ACP Mussa M. Kiswaka; ACP Justin Kaziulaya na ACP Bertha J. Minde.