Tuesday, August 29, 2017

VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA NCHINI VYAITIKIA WITO WA RAIS MAGUFULI KUNUNUA BUTI KATIKA KIWANDA CHA VIATU KARANGA, MOSHI

Mkuu wa Divisheni ya Huduma za Urekebishaji, Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila akisalimiana na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza mara baada ya kuwasili katika ziara Maalum ya kukagua maboresho mbalimbali katika Kiwanda cha Viatu cha Gereza Kuu Karanga Moshi leo Agosti 29, 2017(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Gereza Kuu Karanga – Moshi, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Leonard Mushi.
Mkuu wa Divisheni ya Huduma za Urekebishaji, Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila akiongea na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza Mkoani Kilimanjaro katika Kiwanda cha viatu cha Karanga Moshi(kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Hassan Mkwiche.
Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila akiangalia Buti la Jeshi lililotengenezwa katika Kiwanda cha Viatu Karanga Moshi.
Viatu aina ya Buti za Jeshi zinazotengenezwa katika Kiwanda cha Viatu Karanga Moshi.
Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila akikagua eneo la mradi wa Ubia kati ya Jeshi la Magereza na Mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF ambapo katika eneo hilo kutajengwa mradi wa Kiwanda kipya cha viatu na bidhaa za ngozi katika eneo hilo.
Mkuu wa Divisheni ya Huduma za Urekebishaji, Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila akifyatua tofali zitakazotumika kujengea nyumba za askari katika Gereza Kuu Karanga, Moshi kama inavyoonekana katika picha.

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).