Tuesday, October 9, 2018

KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI AFUNGUA KIKAO CHA BAJETI YA SHIRIKA LA MAGEREZA KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019 MKOANI MOROGORO

Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akisalimiana na Kamishna wa Utawala Gaston Sanga pamoja na viongozi waandamizi wa Jeshi la Magereza alipowasili katika  Ukumbi wa Mikutano wa Mwamvita  Mkoani Mororgoro tarehe 9 Oktoba 2018.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Jacob Gideon Kingu akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike alipowasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwamvita Mkoani Mororgoro.

Mdhibiti Mkuu wa Shirika la Magereza,Naibu Kamishna  Afwilile Mwakijungu akitoa maelezo mafupi kuhusu Shirirka kabla ya mgeni rasmi kukaribishwa kufungua kikao.

Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akitoa maelezo mafupi kabla ya kukmkaribisha Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Jacob Gideon Kingu kufungua kikao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Gideon Kingu akisisitiza jambo kwa Wakuu wa Mikoa ya Kimagereza, Wakuu wa Magereza na Wakuu wa Miradi mbalimbali ambayo iko chini ya Shirika la Magereza, kabla ya ufunguzi rasmi wa Kikao.

  Wakuu wa Magereza na Wakuu wa Miradi mbalimbali ambayo iko chini ya Shirika la Magereza wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na viongozi wakuu wa Jeshi la Magereza nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Gideon Kingu (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa juu wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara. Kulia kwa katibu mkuu ni Kamishna Jenerali Kasike, Kamishna wa Sheria na Utawala wa Magereza Uwesu Ngarama na Kamishna wa Miundo Mbinu na Uzalishaji Tusekile Mwaisabila. Kushoto kwa Katibu Mkuu ni Kamishna wa Utawa na Rasilimali watu Gaston Sanga, Kamishna wa Fedha na Mipango Gideon Nkana na Kamishna wa Huduma za Parol,Viwanda,Huduma za Jamii na Program za Urekebishaji Augustine Mboje.Waliosimama ni Manaibu Kamishna.