Thursday, January 24, 2019

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, PHAUSTINE KASIKE AWASILI JIJINI MBEYA LEO TAYARI KWA ZIARA YA KIKAZI KATIKA BAADHI YA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kulia vazi la kiraia) akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Songwe leo Januari 24, 2019 tayarri kwa ziara ya kikazi katika baadhi ya mikoa ya nyanda za juu kusini ikiwemo Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi na Ruvuma.


Kutoka kulia ni Mkuu wa Gereza Kuu Ruanda Mbeya, SSP Lugona Msomba, Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya awali ya Uaskari Magereza – Kiwira, ACP. Mathias Mkama, Mkuu wa Chuo cha Ufundi Ruanda Mbeya, SSP. Enock Lupyuto kwa pamoja wakiteta jambo kabla ya mapokezi ya Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini leo Januari 24, 2019 jijini Mbeya.


Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(vazi la kiraia) akisalimiana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya mapema  alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Songwe leo Januari 24, 2019 kwa ziara ya kikazi katika baadhi ya mikoa ya nyanda za juu kusini.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(katikati vazi la kiraia) akiteta jambo na Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo mara baada ya kuwasili jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi(kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Mbeya, SACP. Luhende Makwaia(wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya awali ya Uaskari Magereza – Kiwira, ACP. Mathias Mkama(wa pili toka kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Mbeya, ACP. Lyzek Mwaseba.(Picha zote na Jeshi la Magereza).