Tuesday, February 5, 2019

WAZIRI MKUU WA TANZANIA MH. KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA BANDA LA MAGEREZA KATIKA WIKI YA SHERIA JIJINI DODOMA TAR. 02 FEB,2019


Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Khasim Majaliwa akihutubia katika ufunguzi wa wiki ya Elimu ya Sheria ambapo kitaifa yanaendelea kufanyika  Jijini Dodoma, kaulimbiu ni utoaji haki ni jukumu la mahakama na wadau.
Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Khasim Majaliwa akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania  Mh.Profesa Ibrahim Juma Jaji Mkuu wa Tanzania , Mh. Tulia Akson Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dr.B. Mahenge Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakiwa katika matembezi ya ufunguzi wa  wiki ya Sheria yaliofanyika   asubuhi ya tarehe 02 Feb, 2019  Jijini Dodoma ambapo yalianzia katika viwanja vya Mahakama Kuu na kuishia katika viwanja vya Nyerere Squire.
Maafisa wa Jeshi la Magereza kutoka Makao Makuu ya Magereza , Ofisi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma na Gereza Kuu Isanga  wakiwa katika matembezi ya wiki ya elimu ya sheria jijini Dodoma kutoka  kushoto ni Kamishna  wa Magereza anayesimamia Fedha na Mipango  (CP) Gideon Nkana , Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Salum Hussein, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Rajabu Nyange, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza(SACP) Mzee Ramadhan Nyamka, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Chacha Jackson Bina,  Mkuu wa Gereza Kuu Isanga Kamishna Msaidizi wa Magereza(ACP) Keneth Mwambije.
Msemaji wa Jeshi la Magereza nchini Mrakibu wa Magereza (SP) Amina Kavirondo akimpa ufafanuzi  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Khasim Majaliwa kuhusu masuala ya haki na ulinzi wa watoto walioko Magerezani kutokana na Mama zao kukinzana na sharia.
Baadhi ya Maafisa na askari wa jeshi la Magereza wakishiriki katika matembezi ya maadhimisho ya wiki ya sheria Dodoma.( picha na Cpl Mfaume Ally- Jeshi la Magereza)