Monday, September 23, 2019

KAMISHNA JENERALI PHAUSTINE KASIKE ARIDHISHWA NA UJENZI WA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU, GEREZA KUU ISANGA TAREHE 21 SEPT 2019

 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Magereza mkoani Dodoma alipowasili kwenye ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya Maafisa na askari katika Gereza Kuu Isanga, Septemba 21, 2019.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(mwenye miwani) akikagua mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya Maafisa na askari katika Gereza Kuu Isanga,  Septemba 21, 2019. Kulia kwake ni Mkuu wa Magereza mkoani Dodoma, ACP. Keneth Mwambije.

Muonekano wa nyumba takribani 20 ambazo tayari zimejengwa katika mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya Maafisa na askari katika Gereza Kuu Isanga zikiwa katika hatua mbalimbali ya ujenzi.

Tofali za kuchoma zikiwa tayari katika mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya Maafisa na askari katika Gereza Kuu Isanga.

Wafungwa wa Gereza Kuu Isanga wakiendelea na kazi ya ujuenzi katika mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya Maafisa na askari katika Gereza Kuu Isanga ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa program ya Urekebishaji magerezani.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(mwenye miwani) akiangalia mbao zinazotumika katika hatua mbalimbali za ujenzi wa mradi wa nyumba za makazi ya Maafisa na askari katika                               Gereza Kuu Isanga, alipotembelea eneo hilo la ujenzi, Septemba 21, 2019.                                   (Picha zote na Jeshi la Magereza).