Monday, August 11, 2014

Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa Pension wa PPF afanya mazungumzo ya awali kuhusu uwekezaji katika maeneo ya Jeshi la Magereza mkoa wa Dar es Salaam na Mtwara

 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akiongoza Kikao cha Mazungumzo ya Awali na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio(hayupo pichani) kuhusu Uwekezaji katika maeneo ya Jeshi la Magereza Mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio akifanya mazungumzo ya Awali na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja(hayupo pichani) kuhusu Uwekezaji katika maeneo ya Jeshi la Magereza Mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara Agosti 11, 2014 Jijini Dar es Salaam.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia mazungumzo ya Awali na Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw William Erio(hayupo pichani) kuhusu Uwekezaji katika maeneo ya Jeshi la Magereza Mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(katikati) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga(Kushoto) ni Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Magereza, Solomon Urio akifuatilia kwa makini mazungumzo hayo.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja(kushoto) akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio eneo linalofaa Uwekezaji wa Hoteli kubwa ya Kimataifa lililopo Ukonga, Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa PPF amefanya mazungumzo ya Awali na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza kuhusu Uwekezaji katika maeneo ya Jeshi la Magereza Agosti 11, 2014 Jijini Dar es Salaam
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini John Casmir Minja akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio(kulia) mara tu baada ya kufanya mazungumzo ya Awali kuhusu Uwekezaji katika maeneo ya Jeshi la Magereza katika Mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara. Mkurugenzi Mkuu wa PPF amefanya mazungumzo hayo  Agosti 11, 2014 Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).