Wednesday, April 27, 2016

Kamishna jenerali wa magereza nchini afunga rasmi mafunzo ya maafisa wateule daraja la kwanza, mkoani Morogoro

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akikagua Gadi Maalum iliyoandaliwa na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza yalifanyika Aprili 27, 2016 katika Viwanja vya chuo cha Jeshi la Magereza, KPF Mkoani Morogoro.
 
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja katika jukwaa akipokea salaam ya heshima kutoka Gadi Maalum iliyoandaliwa na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza(hawapo pichani).
 Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza wakipita mbele ya Mgeni rasmi katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika Viwanja vya chuo cha Jeshi la Magereza, KPF Mkoani Morogoro.
 
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja(kushoto) akimvisha cheo cha RSM mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza ambaye amefanya vizuri zaidi katika Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa muda wa miezi miwili.

Baadhi ya Maofisa wa Kike wa Jeshi la Magereza ambao ni miongoni mwa wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza kama wanavyoonekana katika picha.
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akitoa hotuba fupi kwa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza(hawapo pichani).
 Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni kama wanavyoonekana katika picha.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akifanya mahojiano na baadhi ya Wawakilishi wa Vyombo vya Habari, Mkoani Morogoro.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza waliosimama mstari wa nyuma
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).