Sunday, January 28, 2018

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, DKT. JUMA MALEWA ATETA NA MAHABUSU GEREZA KEKO MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA NCHINI

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akiwasili katika Gereza la Mahabusu Keko jijini Dar es salaam katika ziara yake ya kikazi kukagua gereza hilo leo Januari 28, 2018 ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria hapa nchini. Jeshi la Magereza ni moja ya wadau muhimu katika sekta ya Sheria hapa nchini. 
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akisalimiana na Mkuu wa Gereza la Mahabusu Keko, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kiangi Abdallah alipowasili katika ziara yake ya kikazi kukagua gereza hilo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria hapa nchini. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo.
Mkuu wa Gereza la Mahabusu Keko, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kiangi Abdallah akitoa taarifa fupi mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa kabla ya kumkaribisha kuongea na Mahabusu wa Gereza Keko(hawapo pichani).
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akiongea na Mahabusu wa Gereza Keko(awapo pichani) leo Januari 28, 2018 alipotembelea gereza hilo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria hapa nchini
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akimsikiliza Mahabusu ambaye ni raia wa kigeni mara baada ya kuongea na Mahabusu wa Gereza Keko.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akikagua jiko la gesi katika Gereza la Mahabusu Keko. Jeshi la Magereza tayari limeanza kutekeleza maelekezo ya Serikali ya kuachana na matumizi ya kuni kwa kutumia nishati ya gesi katika baadhi ya magereza nchini hivyo kutunza mazingira.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiwa katika chumba Maalum, Gereza Keko ambapo chumba hicho kitatumika katika Uendeshaji wa Mashauli mbalimbali kwa kutumia njia ya TEHAMA. Uwepo wa mfumo huu utalipunguzia gharama Jeshi la Magereza katika kuwasafirisha Mahabusu mahakamani na kuwarejesha magerezani.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika Chumba Maalum ambacho kitatumika katika uendeshaji wa mashauli kwa kutumia njia ya  TEHAMA(wa kwanza kushoto) ni  Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Noel James(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Gereza Keko, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kiangi Abdallah 

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).