Monday, January 29, 2018

JESHI LA MAGEREZA LASHIRIKI VYEMA MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA NCHINI, JIJINI DAR

Naibu Kamishna wa Magereza Tusekile Mwaisabila(wa pili toka kushoto) akiwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mussa Kaswaka(wa tatu toka kulia) pamoja na Maafisa wa Jeshi la Magereza  wakishiriki maandamando ya Maadhimisho ya wiki ya sheria. Maandamano hayo yalfanyika jana Januari 28, 2018 yakianzia katika Viwanja vya Mahakama ya Kisutu na kuishia katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Baadhi ya askari wa Jeshi la Magereza wakishiriki katika maandamano hayo jana ambapo yaliongoozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa. Ibrahim Juma.
Baadhi ya Wananchi waliotembela Banda la Jeshi la Magereza wakipata ufafanuzi wa mambo mbalimbali kutoka kwa Maafisa Magereza kuhusiana na Uendeshaji wa Jeshi la Magereza kama inavyoonekana katika picha.

Mrakibu wa Magereza, Amina Kavirondo ambaye ni Mwanasheria kutoka Kitengo cha Sheria Makao Makuu ya Magereza akitoa ufafanuzi kwa kisheria kwa Mwananchi aliyetembelea katika Banda la Magereza katika Viwanja vya Mnazi Mmoja kwenye Maonesho ya wiki ya Sheria hapa nchini.
(Picha zote na Cpl. Mfaume wa  Jeshi la Magereza).