Monday, September 10, 2018

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA PHAUSTINE KASIKE APOKEA MISAADA YA KIBINADAMU YA WAFUNGWA GEREZA KUU KARANGA, MOSHI

Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP)  Phaustine Kasike akisalimiana na Meneja Miradi wa Asasi ya Kidini ya New Life In Christ Ndg. Charles Shang’a mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga Moshi kwa ajili ya hafla fupi ya kupokea Misaada ya Kibinadamu iliyotolewa na Asasi hiyo kwa ajili ya  wafungwa  leo Septemba 8, 2018

Wageni wa meza kuu wakiongzwa na Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP)  Phaustine Kasike (katikati)  wakiimba wimbo wa Taifa la Tanzania ikiashiria ufunguzi wa hafla fupi ya kupokea misaada ya Kibinadamu kwa ajili ya wafungwa iliyotolewa na Asasi ya Kidini ya New Life In Christ. Tukio hilo limefanyika leo Septemba 8, 2018 katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga Moshi.

Mkurugenzi wa Asasi ya Dorcas Aid International Tanzania  Bi. Lilian Urasa akitoa maelezo mafupi kabla ya kukabidhi msaada wa Kibinadamu kwa ajili ya Wafungwa nchini. Dorcas Aid International Tanzania hushirikiana na Asasi ya Kidini ya New Life In Christ katika kutoa misaada ya namna hiyo.

Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP)  Phaustine Kasike akipokea msaada wa vyerehani uliotolewa  na Asasi ya Kidini ya New Life In Christ leo Septemba 8, 2018 kwa ajili ya wafungwa. Hafla ya upokeaji wa misaada hiyo imefanyika katika gereza Kuu Karanga Moshi


Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP)  Phaustine Kasike (wa pili kushoto) akipokea msaada wa vifaa vya kuchomelea akiwa ni sehemu ya vifaa vilivyotolewa na Asasi ya Kidini ya New Life In Christ kwa ajili ya wafungwa vitakavyotumika kuwafundisha stadi mbalimbali za ufundi magerezani.

Mwenekano wa baadhi ya  misaada ya Kibinadamu  iliyotolewa Asasi ya Kidini ya New Life In Christ iliyokabidhiwa kwa Jeshi la Magereza leo Septemba 8, 2018 katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga Moshi. Misaada iliyotolewa leo kwa ujumla wake ina thamani ya zaidi ya milioni 200.2.


Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP)  Phaustine Kasike (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya askari wa magereza mkoani Kilimanjaro wakati wa hafla ya kupokea misaada ya Kibinadamu kutoka kwa Asasi ya Kidini ya New Life In Christ leo Septemba 8, 2018. Kutoka kulia ni Miradi wa Asasi ya Kidini ya New Life In Christ Ndg. Charles Shang’a, Mkurugenzi wa Asasi ya Dorcas Aid International Tanzania  Bi. Lilian Urasa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Dkt. Hasan Mkwiche. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Emmanuel Lwinga, Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Anderson Kamtiaro na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Hamis Isaya.

Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP)  Phaustine Kasike akitoa hotuba kwa wageni mbalimbali (hawapo pichani) waliohudhuria hafla fupi ya kupokea msaada wa Kibinadamu kwa ajili ya wafungwa  kutoka kwa Asasi ya Kidini ya New Life In Christ  leo Septemba 8, 2018 katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga Moshi.

Kikundi cha Sanaa cha Mama Jusi Anglikan cha mjini Moshi kilikonga nyoyo za wageni waalikwa katika hafla ya kupokea msaada wa Kibinadamu uliotolewa na Asasi ya Kidini ya New Life In Christ leo Septemba 8, 2018.