Monday, September 10, 2018

KAMISHNA JENERALI KASIKE AFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOANI TANGAKamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike akifuatilia kwa makina taarifa ya mkoa wa Tanga kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Magereza wa Mkoa huo Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Emmanuel Lwinga alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja mkoani humo leo Septemba 7,2018.


Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike (mwenye miwani) akisalimiana na baadhi ya maafisa wa ofisi ya Mkuu wa Magereza mkoa wa Tanga, Gereza Kuu Maweni na gereza la Mahabusu Tanga  mara alipowasili katika viwanja vya Gereza Kuu Maweni jijini Tanga  akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja  mkoani humo leo Septemba 7, 2018.
Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya askari wa Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani (KMKGM) walioko mkoani Tanga alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja mkoani humo leo Septemba 7, 2018.

Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike (mwenye “microphone” ) akizungumza na maafisa na askari wa vituo vya ofisi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Gereza Kuu Maweni na Gereza la Mahabusu Tanga (hawapo pichani) kwa pamoja katika bwalo la Gereza Kuu Maweni Tanga alipofanya ziara ya siku moja ya kikazi mkoani humo. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Emmauel Lwinga, wa tatu kulia ni Mkuu wa Gereza Kuu Maweni Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Felichism Masawe na wa kwanza kushoto ni Afisa Mnadhimu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Marakibu Mwandamizi wa Magereza (SSP) Hamis Mbwana.

Baadhi ya maafisa na askari  wa  vituo vya ofisi ya Mkuu wa Magereza mkoa wa Tanga,  waliokusanyika kwa pamoja katika bwalo la gereza Kuu Maweni  wakifuatilia kwa makini hotuba ya Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (hayupo pichani)  alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo leo  Septemba 7, 2018. Katika hotuba yake CGP ametilia mkazo suala la kubadili mtazamo wa kiutendaji, kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili kufanikisha majukumu yetu kama serikali na jamii nzima inavyotarajia kutoka kwetu.

Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike akiwa katika picha ya pamoja na baadhi askari wa magereza wa kike mkoani Tanga alipofanya ziara ya siku moja mkoani humo leo Septemba 7, 2018.
Picha zote na Jeshi la Magereza.