Thursday, May 14, 2020

SERIKALI YARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI BODI ZA PAROLE NCHINI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Hamad Masauni(Mb) akitoa hotuba katika hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi ya Taifa Parole Taifa, leo Mei 14, 2020 katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango, jijini Dodoma.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee ambaye pia ni Katibu wa Bodi ya Taifa Parole akitoa maelezo mafupi kuhusiana na utendaji kazi wa Bodi za Parole nchini tangu kuanzishwa kwake mwaka 1994. Leo Mei 14, 2020 katika hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi ya Taifa Parole Taifa, katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango, jijini Dodoma.

Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia uzinduzi wa Bodi ya Taifa Parole leo Mei 14, 2020 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Parole Taifa, Mhe. Dkt. Augustino Mrema akisoma taarifa fupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi azindue Bodi ya Taifa Parole leo Mei 14, 2020 jijini Dodoma.

Mjumbe wa Bodi ya Taifa Parole, Mchungaji wa Kanisa la KKKT  Dodoma, Marco Kinyau akijitambulisha mbele ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Hamad Masauni(Mb) kabla ya uzinduzi wa Bodi ya Taifa Parole leo Mei 14, 2020 jijini Dodoma. Kulia kwake ni baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo.

Meza kuu wakifuatilia utambulisho wa wajumbe wapya wa Bodi ya Taifa Parole. Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Hamad Masauni(kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee(kushoto) ni Mwenyekiti wa Parole Taifa, Mhe. Augustino Mrema.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Hamad Masauni(meza kuu katikati aliyeketi) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Taifa Parole(waliosimama). Wa pili toka kulia aliyeketi meza kuu ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee (Wa pili toka kushoto aliyeketi meza kuu) ni Mwenyekiti wa Parole Taifa, Mhe. Augustino Mrema.
 (Picha zote na Jeshi la Magereza).