Friday, May 8, 2020

WAZIRI MAVUNDE AMWAGA MISAADA YA VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORANA GEREZA KUU ISANGA, DODOMA

Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee(kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde (Mb) leo Mei 8, 2020 alipofika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza jijini Dodoma kabla ya kukabidhi vifaa vya kujikinga na janga la corona katika Gereza Kuu Isanga Dodoma.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee (kushoto meza kuu) akizungumza jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde (kulia) leo Mei 8, 2020 alipofika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza jijini Dodoma kabla ya kukabidhi vifaa vya kujikinga na janga la corona katika Gereza Kuu Isanga.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza nje ya Gereza akikabidhi vifaa vya kujikinga na janga la corona katika Gereza Kuu Isanga, jijini Dodoma. Mhe. Mavunde amekabidhi msaada uliojumuisha vifaa mbalimbali ikiwemo sabuni, ndoo za maji pamoja na  vitakasa mikono (Sanitizer).

Baadhi ya vifaa hivyo vilivyokabidhiwa katika Gereza Kuu Isanga na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde.

Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma, ACP. Keneth Mwambije akimshukru Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde (kushoto) baada ya kupokea msaada wa vifaa vya kujikinga na janga la corona.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee( wapili kushoto) akiagana na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde mara baada ya mazungumzo katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, jijini Dodoma.                                              (Picha zote na Jeshi la Magereza).