Friday, November 14, 2014

Taarifa kwa vyombo vya habari

Tarehe 17 Novemba, 2014 saa 4:00 asubuhi Jeshi la Magereza litapokea msaada wa vifaa vya ujenzi na vitendea kazi vitakavyotumika katika ujenzi wa makazi ya Maafisa na Askari wa Gereza Wazo. Tukio ambalo litafanyika katika Viwanja vya Gereza Wazo, Wilayani Kinondoni, Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa leo na Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini msaada huo umetolewa na Kampuni ya Twiga Cement ya Jijini Dar es Salaam kufuatia kusainiwa kwa Makubaliano ya kuiuzia Kampuni hiyo madini ya chokaa katika eneo la Gereza Wazo.

Mgeni rasmi katika tukio hilo atakuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias M. Chikawe(Mb). Aidha, Wadau mbalimbali toka nje ya Jeshi la Magereza watakuwepo katika hafla hiyo.

Kuanza kwa mradi wa ujenzi wa nyumba hizo utapunguza tatizo la muda mrefu la uhaba wa Nyumba zenye hadhi kwa ajili ya makazi ya Maafisa na askari wa Gereza hilo.


Vyombo vya Habari vinakaribishwa kwenye shughuli hiyo katika muda ulioelezwa.


Imetolewa na;
Lucas A. Mboje, Mkaguzi wa Magereza;
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza;
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza;
DAR ES SALAAM.
14 Novemba, 2014.