Thursday, November 20, 2014

Uzalishaji wa mifugo katika mashamba ya Jeshi la Magereza waongezeka kwa mafanikio makubwa nchini

Sehemu ya Wanyama kazi katika Shamba Kubwa la Uzalishaji wa ngo'mbe wa nyama katika Gereza Ubena lililopo Mkoani Pwani. Shamba hilo lina takribani jumla ya ngo'mbe zaidi ya 1500. Uzalishaji wa ngo'mbe umekuwa ukiongezeka kwa mafanikio makubwa kila Mwaka hivi karibuni kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Uongozi wa Jeshi la Magereza katika kuyahudumia mashamba hayo Nchini.
Lango Kuu la kuingilia Gereza la Mifugo Ubena lililopo Mkoani Pwani ambalo linashughulika zaidi na Uzalishaji wa Mifugo. Wafungwa katika Gereza hilo wanapata elimu ya Ufugaji bora unaozingatia Kanuni za Ufugaji wa Kisasa ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa jukumu la Urekebishaji kwa Wafungwa.
Kundi la ndama wakiwa zizini katika Shamba la Uzalishaji wa Mifugo Gereza la Mifugo Ubena, Mkoani Pwani.
Kundi la ngo'mbe wa maziwa katika Shamba la Mifugo la Mtego wa Simba lililopo Mkoani Morogoro. Shamba hili la Mifugo ni Maalum kwa Uzalishaji wa Ngo'mbe wa maziwa kama inavyoonekana katika picha na Gereza hilo lilianzishwa rasmi mwaka 1944.
Maziwa yakiwa tayari yamekamliwa na kuhifadhiwa kwenye majokovu kabla ya kwenda kwa walaji. Shamba hilo la Uzalishaji ngo'mbe wa maziwa la Gereza Mtego wa Simba limekuwa likipigiwa mfano hapa nchini

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).