Sunday, March 13, 2016

Kamishna Jenerali Minja atembelea kambi maalum ya wakimbizi kutoka Burundi inayosimamiwa na jeshi la Magereza pamoja na shamba la mifugo gereza Kitengule, mkoani Kagera

Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP John Casmir Minja akisalimiana na Mkuu wa Kambi ya Utenganisho Mwisa, SP. S. Lubinza alipotembelea katika Kambi hiyo Machi 12, 2016 kisha kuongea na Wakimbizi kutoka Burundi ambao wanazuiliwa katika Kambi hiyo kwa mujibu wa Sheria.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP John Casmir Minja pamoja na ujumbe wake aliofuatana nao akikagua sehemu mbalimbali za Kambi hiyo ili kuona kama zinakidhi viwango vinavyokubalika katika kuwahifadhi Wakimbizi hao ambao wanahifadhiwa katika Kambi hiyo.
Askari Mlinzi kutoka Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza akiwa timamu kiulinzi kama anavyoonekana katika eneo lake la kazi ili kuhakikisha Ulinzi na Usalama wa Kambi hiyo Maalum iliyopo Mkoani Kagera.
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP John Casmir Minja(katikati) akiongea na Wakimbizi kutoka nchini Burundi(hawapo pichani) ambao wanahifadhiwa katika Kambi hiyo Maalum kwa sababu za kiusalama.
Sehemu ya kundi la ngo'mbe wa maziwa na nyama wakiwa zizini katika Shamba la Mifugo linalomilikiwa na Jeshi la Magereza katika Gereza la Kilimo Kitengule lililopo Mkoani Kagera.
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP John Casmir Minja akikagua ujenzi unaoendelea wa Jengo la Banda la ndama katika  Shamba la Mifugo linalomilikiwa na Jeshi la Magereza katika Gereza la Kilimo Kitengule lililopo Mkoani Kagera alipotembelea katika ziara yake ya kikazi Machi 12, 2016.
Kundi la ndama wakiwa zizini katika Shamba la Mifugo linalomilikiwa na Jeshi la Magereza katika Gereza la Kilimo Kitengule.

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza)