Monday, March 14, 2016

Waziri mkuu Kassim Majaliwa ampongeza kamishna jenerali wa magereza kwa namna anavyosimamia utendaji kazi mzuri wa jeshi hilo nchini

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa(MB) alipotembelea Kambi Maalum ya Mwisa inayohifadhi Wakimbizi kutoka nchini Burundi leo Machi 14, 2016
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa(MB)akitoa hotuba yake fupi kwa Maafisa na askari wa  wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) kutoka vituo mbalimbali vya Magereza yaliyopo Mkoa wa Kagera alipotembelea Kambi ya Utenganisho ya Mwisa leo Machi 14, 2016.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa umakini mkubwa hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa(hayupo pichani).
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akitoa taarifa fupi ya Hali ya Magereza nchini mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa(hayupo pichani).
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Masauni akitoa neno fupi kabla ya kumkaribisha rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kutoa hotuba yake fupi.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kagera, SACP. Omari (aliyesimama kushoto)  taarifa fupi ya Wambizi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiongea na Wakimbizi(walioketi chini) katika Kambi ya Mwisa inayosimamiwa na Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Shirika la kuwahudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR).
Msafara wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ukiondoka katika Kambi ya Mwisa iliyopo Mkoani Kagera


WAZIRI MKUU  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amempongeza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja kwa utendaji wake mzuri wa kazi kwa namna anavyosimamia kikamilifu utekelezaji wa majukumu wa Jeshi hilo.

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri Mkuu  kwenye ziara yake  Mkoani Kagera aliyoifanya katika Kambi ya Utenganisho ya Mwisa inayoendeshwa na Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Shirika la kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR).

"Nampongeza sana Kamishna Jenerali Minja hususani kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuhakikisha kuwa  Jeshi la Magereza linaendelea kutekeleza kikamilifu majukumu yake kwa kuzingatia Sheria za Magereza mbali na changamoto kadhaa zinazolikabili Jeshi hilo ikiwemo Msongamano mkubwa uliopo Magerezani." Alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Aidha, ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamilia kutatua baadhi ya changamoto mbalimbali zinazokabili Jeshi hilo ili kuwezesha ufanisi zaidi wa utekelezaji wa majukumu yake. 

Awali akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu  kwenye ziara yake  Mkoani Kagera aliyoifanya katika Kambi ya Utenganisho ya Mwisa, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja alisema kuwa Jshi la Magereza linakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo kwa kiasi fulani zinaathiri utekelezaji wa majukumu yake.
 
Jenerali Minja alizitaja baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na Msongamano wa wafungwa Magerezani, ufinyu wa bajeti, makazi duni ya Maafisa n askari, uhaba wa vitendea kazi, uhaba na uchakavu wa vyombo vya usafiti na mawasiliano, ukosefu wa pembejeo, ukosefu  wa Magereza katika baadhi ya Wilaya mpya zinazoanzishwa kiutawala. 

Aidha,  Jenerali Minja amesema kuwa katika kukabiliana na changamoto hizo, Jeshi la Magereza limekuwa likifanya jitihada mbalimbali na za makusudi kwa kufanya maboresho katika maeneo kadhaa ili kujiongezea tija na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa yupo Mkoani Kagera kwa lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani humo ambapo katika ziara yake pia ameweza kuitembelea Kambi ya Mwisa inayohifadhi Wakimbizi kutoka nchini Burundi.(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).