Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya Ukimwi, ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Hassan Mtenga, imefanya ziara ya ukaguzi katika Zahanati ya Gereza Singida, leo machi 17, 2025, ikiwa na lengo la kutathmini huduma zinazotolewa zahanati hapo.
Katika ukaguzi huo Kamati ilikagua huduma za CTC, chumba cha Maabara, chumba cha daktari, chumba cha takwimu pamoja na chumba cha dawa, pia waliweza kufanya kikao na Kamati ya mkoa ya Afya na masuala ya Lishe na kuupongeza uongozi wa jeshi la magereza kwa huduma wanazotoa katika zahanati hiyo.
"Hongereni kwa kazi kubwa na nzuri ambayo mnafanya, tumejionea , DMO pamoja na dactari mkuu wa mkoa tunaomba mtatue changamoto ndogondogo zinazokabili zahanati ya gereza" alisema Mhe. Mtenga
Aidha Mhe. Mtenga ametoa rai kwa Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na wabunge wote nchini kujenga utamaduni wa kutembelea Magereza mbalimbali ili kubaini changamoto zinazoyakabili na kuzitafutia ufumbuzi.
Kwaupande wake Kamishina Jenerali wa Magereza Jeremia Yoram Katungu ameishukuru Kamati ya Bunge ya Afya na Masuala ya Ukimwi kwa kutembelea na kukagua Zahanati hiyo na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote waliyoyatoa ili kuboresha huduma za Afya